Pundamilia ni moja katika alama
za barabarani.Alama hii ina maana ni sehemu ya kuvuka waenda kwa miguu na
magari hutakiwa kusimama.Nimekuwa nikishangazwa mara kwa mara kusoma kuhusu
watu kugongwa na magari katika alama hizi.Nimeshuhudia mwenyewe vilevile jinsi
madereva wanavyokaidi kusimama katika alama hizi.Madereva wanapita kama vile
hakuna alama yeyote.Hii inasikitisha sana.Maana inaleta maana kuwa barabara ni
haki ya waendesha vyombo vya moto na si kwa watembea miguu. Sweden,alama za
barabarani zinaheshimika mno.Madereva wanazingatia sana mwendokasi ulioweka
mfano katika eneo la shule ambapo magari hutakiwa kutembea si zaidi ya kilomita 30 kwa saa. Kwenye alama ya
pundamilia,hata kama wewe mvuka kwa miguu utaona gari inakuja na kuwa na shaka kuwa dereva atapita,huwa
haiwi hivyo.Dereva atasimama na kukuonyesha ishara ya kuvuka! Sweden, kosa la dereva kuzembea katika alama za
barabarani hupelekea dereva huyo kufungwa jela na kupoteza leseni. Na hata
ukitaka kupata leseni tena baada ya kutumikia adhabu inabidi ufuate taratibu
upya kama mtu asiyekuwa na leseni.Taratibu zenyewe zina mlolongo mrefu na
ni gharama.
Inasikitisha nchini kwetu kuona
watoto wa shule wanagongwa na kufa tena nje ya shule zao.Hivi hawa wanaogonga
watoto na raia wengine katika alama za pundamilia huchukuliwa hatua gani?Au
ndiyo marehemu hana haki?
Nadhani imefikia wakati wa kubadilishwa kwa sheria za barabarani zisizokidhi nchini Tanzania.Nina imani sheria ngumu zitapunguza sana ajali za barabarani.
Je,sheria zetu zikoje?
No comments:
Post a Comment