Wanawake wanakwenda umbali mrefu kutafuta maji
Marehemu Zuhura Juma ambaye aliuliwa na mumewe huko Tabora
Leo ni siku ya wanawake duniani.Siku hii ni ya kufanya
tathmini kwa maisha ya wanawake wote duniani ikiwemo kuangalia haki zao za
msingi kama zinapatikana. Haki hizo ni kama uzazi salama, kutokuwepo ukatili wa
kijinsia dhidi yao n.k.
Bado tunashuhudia kuwa wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa
katika familia nyingi.Wanawake ndiyo walezi wa watoto. Wanawake wanafanyiwa
ukatili kila siku ikiwemo kutelekezwa na watoto, kupigwa, kubakwa na kutumika
kama chombo cha uzalishaji(kuleta kipato katika familia). Katika nchi nyingi
masikini na zinazoendelea,huduma ya uzazi/afya kwa wanawake ni duni hivyo
kupelekea wengi kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Wanawake wa vijijini ndiyo wanapata adha zaidi. Je msomaji,unapenda
kutoa mawazo gani juu ya siku hii?Ni lini mwanamke atapata ukombozi wa kweli?
Ni lini atapata usawa anaouhitaji?
Imeandikwa na Anna Nindi
HAPPY WOMEN´S DAY!
No comments:
Post a Comment