Nikiwa Tunduru nilishtushwa sana
na hadithi za simba waliokuwa wakijitokeza mara kwa mara mjini Tunduru. Hii
siyo hadithi, ni matukio ya kweli.
Kipindi nilichokuwepo Tunduru
ilikuwa ni mwezi wa Desemba na tukakuta stori kuwa mwezi wa septemba,simba
aliingia mjini!Mdau, ingekuwa ni wewe katika mazingira haya ungejisikiaje?
Yaani unapewa habari hizi siku ya kwanza tu kufika sehemu ambayo utakaa mwezi
mzima!Kwa kweli taarifa hii ilininyima raha kabisa maana wakati mwingine
tulikuwa tunamaliza kazi zetu usiku.Sehemu tuliyokuwa tunakaa ilikuwa karibu
sana na eneo letu la kazi ila ilitubidi tuwe na usafiri tukitoka usiku.
Palikuwa na msikiti jirani na msikiti huo ulisaidia sana kutoa matangazo
mbalimbali wakati wa swala mchana au usiku, hususan kuhusu watoto waliopotea au
kama simba kaonekana mjini.
Sijui kwasasa hali hiyo ya simba
kuvamia makazi ya watu imekwisha au bado ni hivyo hivyo?
KWA KWELI TEMBEA UONE!
Imeandikwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment