Nilitembelea Turiani iliyopo
katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.Turiani kunasifika kwa kilimo cha miwa
na ndiyo kuna kiwanda cha sukari cha Mtibwa.Wakazi wa Turiani ni wakulima.
Asubuhi moja tukielekea katika shughuli iliyotupeleka pale,tukakutana na kijana
anauza ndizi mbivu katika sinia kubwa alilobeba kichwani. Ndizi zilikuwa nzuri
sana kwa kweli. Nilimuuliza bei ya ndizi. Bei aliyotutajia Yule kijana mimi na
mwenzangu tukatazamana na kushangaa.
Alipoona tumeshangaa kijana Yule akasema, “mshishtuke na bei,mnaweza kuomba heri”. Tukamuuliza kivipi? Akatujibu “Naona mmeshtuka nauza ghali,naweza kuwapunguzia bei.
Alipoona tumeshangaa kijana Yule akasema, “mshishtuke na bei,mnaweza kuomba heri”. Tukamuuliza kivipi? Akatujibu “Naona mmeshtuka nauza ghali,naweza kuwapunguzia bei.
Kilichotushtusha ni bei aliyotaja
ilivyokuwa ndogo nab ado muuzaji alikuwa tayari kupunguza bei!
Tukagundua neno “kuomba
heri” lilimaanisha “kupunguziwa bei”.Tulisikitika kuwa kijana Yule alikuwa
anazunguka na sinia la ndizi ambalo kipato chake wala kisingekidhi mahitaji
yake nabado alikuwa tayari kutupunguzia bei.
Tulimwambia tutatununua tu kwa
bei anayouza bila ya kuomba heri.Tulinunua ndizi zake zote na kupelekea wenyeji
wetu wale kila mtu kwa uwezo wake.
KWELI TEMBEA UONE!
Imeandikwa na
Anna Nindi
No comments:
Post a Comment