Friday 15 May 2015

JE,UNAUJUA MSWAKI? SOMA HAPA

Miswak
Mswaki (inatokana na neon la  Kiarabu miswaq), ni kijiti kibichi ambacho kinatokana na mti au kichaka na kisha kutafunwa upande mmoja na  hutumika kusafishia meno kutokana na mabaki ya chakula yanayoweza kuyaharibu.
FAIDA ZA MSWAKI
Inasemekana mswaki unaimarisha ufizi (nyama inayoshikili meno), unazuia uozo wa meno, unaondoa maumivu ya meno na harufu mbaya kinywani.



Hasa ukitokana na mti mswaki (Salvadora persica) (arak kwa Kiarabu) au miti mingine maalumu kulingana na mazingira, kwa mfano msega au mkupa (Dobera glabra na D. loranthifolia), una sifa za muda mrefu zinazoufanya uendelee kuwa mbadala wa miswaki ya kisasa, ikiwepo ile inayotumia umeme.
Unatumika hasa Uarabuni, Afrika Kaskazini, kwenye Sahel na Pembe ya Afrika, India, Asia ya Kati, Asia ya Kusini Mashariki.

KAULI YA WANASAYANSI
World Health Organization (kifupi WHO, yaani Idara ya Afya ya Umoja wa Mataifa) ilihamasisha matumizi ya mswaki mwaka 1986.

Mwaka 2000 ripoti ya kimataifa kuhusu usafi wa kinywa ilionyesha makubaliano ya kwamba unahitajika utafiti zaidi kuthibitisha faida ya mswaki.
Utafiti wa mwaka 2003 ulionyesha kwamba matumizi sahihi ya mswaki asili yalikuwa na manufaa kuliko miswaki ya kisasa. Hata hivyo, utafiti uliishia kupima watu 15 tu, idadi isiyotosha kabisa kama uthibitisho.

Matumizi
Ingawa wengi wanapiga mswaki hasa asubuhi wanapooga au kunawa, halafu pengine huenda wakanywa chai ambayo inaacha sukari katika meno na hivyo kuandaa uozaji wake, utaratibu sahihi ni kupiga mswaki baada ya chakula, hasa cha jioni, kusudi meno yabaki safi muda wote wa usiku.

Kwa kulinda usafi, ncha ya mswaki inatakiwa kukatwa kila unapotumika.

Usitunzwe kamwe karibu na choo au sinki.

Mswaki ukikauka unatakiwa kulainishwa kwa maji ya waridi.
CHANZO: Wikipedia

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...