Monday, 11 May 2015

SUPU YA NYAMA YA KUSAGA NA MBOGAMBOGA

Hii supu ni rahisi sana kutengeneza na ina virutubisho vyote.Ni mlo wangu sa mchana wa leo.Ninakuandikia hapa upishi wake.

MAHITAJI( kwa watu 2)

½-1 kikombe Nyama ya kusaga
Pilipilimanga (weka kiasi upendacho)
Chumvi (weka kiasi upendacho)
Mbogamboga nilizotumia
1 kitunguu maji
1 Karoti(ukubwa wa wastani)
¼ kikombe njegere
¼ kikombe French beans
1 kiazi chenye ukubwa wa kati


FANYA HIVI
  • Katakata karoti, kiazi na kitunguu katika vipande vidogo vidogo
  • ·         Weka nyama ya kusaga katika sufuria.Weka jikoni na acha nyama ichemke.
  • ·         Tumbukiza mbogamboga zote ziendelee kuchemka na nyama.
  • ·         Pika mpaka uone viazi vimelainika.
  • ·         Weka chumvi na pilipilimanga kupata ladha

Supu yako ipo tayari na unaweza kula yenyewe tu na ukashiba au ukala na chapati au mkate. 

ANGALIZO: Mbogamboga unaweza kutumia unazopenda kama: kabichi, brokoli, hoho n.k

Mpishi: Anna