Mandhari nzuri ya nyumba
huchangiwa na vitu vingi ikiwamo na mpangilio mzuri wa jiko. Jiko hutakiwa
kujengwa kukidhi mahitaji yote ya jikoni. Kila kitu hutakiwa kuwa mahali
pake,kuanzia vyombo hadi mashine ndogo za jikoni.Unaweza ukawa umejengewa jiko
vizuri sana ila wewe mwenyewe usiwe na uwezo wa kupanga vitu vyako vizuri
ukaweka sufuria hapa,sahani pale,blender hapa,matunda yametapakaa tu kwenye meza za jikoni, vyombo vichafu vimejaa tele katika sinki, ili mradi mtu akiingia anaona
kama vile yupo stoo badala ya jikoni.Jikoni kunatakiwa kuwe safi muda wowote na
ikibidi mtu akiingia asijue kabisa mmekula nini!Maana kuna majiko ukiingia
unajua kabisa hawa leo wamekula samaki n.k! Unaweza usisikie harufu bali kukawa na
mabaki labda katika sinki au vyote kwa pamoja ( yaani mabaki na harufu).
Angalia picha zifuatazo utaona
jinsi jiko linavyotakiwa kuonekana muda wote.Kazi kwako!
No comments:
Post a Comment