Friday, 19 June 2015

DUNIANI KUNA MAMBO: VITUKO UGHAIBUNI: JAMAA AZIGAWA MALI ZAKE NUSU KWA NUSU BAADA YA KUMWAGANA NA MKEWE

Baiskeli iliyokatwa na jamaa huyo.
Gari hili nalo lilikatwa katikati kwa ajili ya kumaliza mgogoro kati ya jamaa huyo na mkewe.
Video ya jamaa huyo akikata mali zake katikati

NJEMBA mmmoja nchini Ujerumani amezua sintofahamu baada ya kuamua kugawa nusu kwa nusu kila mali…
Baiskeli iliyokatwa na jamaa huyo

Gari hili nalo lilikatwa katikati kwa ajili ya kumaliza mgogoro kati ya jamaa huyo na mkewe.
Video ya jamaa huyo akikata mali zake katikati.


NJEMBA mmmoja nchini Ujerumani amezua sintofahamu baada ya kuamua kugawa nusu kwa nusu kila mali aliyokuwa anamiliki ili kumalizana na mkewe mara baada ya kuachana.

Katika video iliyowekwa Youtube ikiwa na kichwa cha habari cha 'Kwa Laura' mwanaume huyo ambaye hakutaja jina lake anaonekana akikata nusu kwa nusu simu aina ya iPhone 5, TV, kiti, kitanda na mwishowe gari.
Kwa kutumia vifaa mbalimbali vikiwemo vya umeme na kisu, mwanaume huyo anaonekana akikata mali zake katika vipande viwili.

"Mke wangu alitaka vitu vingi ambavyo nimevipata kwa jasho langu. Hivyo nimeamua kugawa katikati kila kitu ninachomiliki ili apate nusu na mimi nusu" aliandika bwana huyo.
Vitu vingine ambavyo alivigawa bwana huyo ni pamoja na Laptop aina ya Macbook Pro, sofa, baiskeli na mdoli.


Video hiyo imejizolea umaarufu ikiwa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 1.2 ndani ya siku tatu baada ya kuwekwa Juni 16, mwaka huu.

Baada ya jamaa huyo kuvigawa vitu hivyo nusu alimpatia mkewe huyo huku nusu yake akiweka katika mtandao wa kuuza bidhaa kupitia internet wa eBay kwa ajili ya kuviuza.
(Credit: Globalnews.ca)