Sunday, 14 June 2015

WANAWAKE NA UJASIRIAMALI

Unaweza pika chapati ka hizi na kuuza

 Wanawake wengi wamejikwamua kutokana na shughuli za ujasiriamali. Ili uwe mjasiriamali si lazima uwe na mtaji mkubwa kwani zipo shughuli nyingi sana ambazo mtu anaweza kufanya kwa kipato kidogo tu.Kinachohitajika hapa ni uvumilivu, nidhamu ya biashara  pamoja na moyo wa kujifunza.
Unaweza tengeneza maandazi kama haya  na kuuza

Ngoja nitoe mfano. Mama unaweza kuwa na pesa zako shilingi za kitanzania 50,000:- na ndoto yako ni kufanya biashara ya mama ntilie. Hapa usianze moja kwa moja biashara ya kupika mamantilie kwani pesa haitakutosha, badala yake unaweza kuanza kupika vitafunwa kama chapatti, maandazi na vitumbua na kuanza kuuza.Usifikirie kupanga sehemu ya biashara au kuajiri mtu mwingine, badala yake tengeneza vitu vyote wewe mwenyewe,nyumbani kwako.Hii yote ni katika kujenga uwezo kwanza,yaani kukuza mtaji na kupata wateja zaidi. 
Mtaji ukikua taratibu unaweza kuongeza chai ya viungo(jitahidi kuwa mbunifu kujifunza toka kwa wengine). Na siku zinavyokwenda ongeza kitu kimoja kimoja mpaka unakuwa full mama ntilie kama ulivyota! Mbona inawezekana tu ukiwa na nia.
Tujaribu kuangalia fursa zinazotuzunguka kwani ndiyo ambazo hutupa mwongozo wa nini tunaweza kujishughulisha nacho.
Nadhani nimeeleweka.
Imeandikwa na  Anna Nindi
Mmiliki wa rainbow-tz blog