Thursday 16 July 2015

ATM YA MAJI YAZINDULIWA KENYA

 
Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa wanaweza kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi mengine.
Mpango unaoungwa mkono na serikali umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi unaowawezesha watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa kutumia kadi.


Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa bei nafuu.

null
Wenyeji wa mitaa ya mabanda nchini Kenya wamekuwa na tatizo la kupata maji safi ambapo hulazimika kununua maji kwa bei ghali kutoka kwa wauzaji au kutoka kwa magenge ambayo hudhibiti na kuuza maji hayo kwa kuyachuuza.
Mradi kama huo umefaulu katika baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni mara ya kwanza kuzinduliwa katika mji huo mkuu.

null
Vituo hivyo vya kutoa huduma hiyo ya maji vimefanikiwa kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya mitaa nchini Kenya na kampuni ya maji ya Grundfos ya Denmark.
Kampuni ya kusimamia huduma ya usambazaji maji, ina mikakati ya kuhakikisha kuwa huduma hii walioianzisha itasambazwa kote katika mji mkuu wa Nairobi na kwengineko nchini humo.

null
Huku hilo likianzishwa wakaazi wa mitaa kadhaa mjini Nairobi bado wanalalamikia ukosefu wa maji.

CHANZO: BBC swahili
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...