Skip to main content

MABIBI ARUSI KUWENI MAKINI NA UTAPELI HUU

Ni vizuri tutumie blog zetu kuelimishana pale panapokuwa na kitu ambacho hakina matokeo mazuri kwa jamii inayotuzunguka.
Hawa ndugu zetu Wachina wamezidi kwautapeli.Kwasasa wana mitandao mingi ambayo wanauza nguo za arusi ambazo ni chini ya kiwango. Wanachofanya ni kupiga picha nguo ya kutoka kwa mbunifu mkubwa na kuweka katika tovuti yao na kuonyesha kuwa ni wao wanaoshona nguo hiyo. Ujanja wao wanaweka bei ndogo kiasi ambacho kwa mtu wa kushtuka atashtuka tu.
Watu wengi wamelizwa nao kwa kweli kwani kutokana na udogo wa budget zao za arusi hukimbilia huku kununua nguo wakidhani kuwa nguo ni rahisi ila wanachokutana nacho ni utapeli.Na matapeli hawa wa China wanatumia anwani za UK ili kujipatia wateja.Kama upo makini angalia namba za simu na utagundua ni Mchina Hahaha.Unaambiwa ukiwa mwongo usiwe msahaulifu! Wanadanganya anwani ila katika nmaba za simu wanaandika za Uchinani!
Ukitaka kununua nguo za jioni arusi usihangaike na hizi tovuti za Wachina.Uliza watu wanaojua wakusaidie au nenda katika maduka yaliyopo mahali unapoishi ukanunue hata kama ni ghali.Vinginevyo kama bajeti imebana sana nenda kakodishe!

Hebu tuangalie baadhi ya nguo na wapi zimetoka.

Kushoto ni nguo halisi kutoka kwa mbunifu mkubwa na kulia ndiyo mnunuzi aliyoletewa

okdress.co.uk
Hawa wanaojiita okdress wameweka picha ya kushoto katika tovuti yao na kulia ndicho mteja alichokumbana nacho.


Utapeli mwingine hapo juu kutoka JJS House


Hapa napo kapigwa mtu kutoka www.audresses.com.Ukiangalia tu utagundua ipi ni gauni halisi na ipi ni fake


Hawa nao ni Dhgate

Ebay nao hawako nyuma!

Hivyo mdau kuwa makini.Unaweza kuingia hapa kusoma zaidi


Natumaini nitakuwa nimeokoa wengi!

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.