Wednesday, 1 July 2015

THE GARDEN: UREMBAJI WA BUSTANI

Unaweza kuwa na bustani yenye maua mazuri na mpangilio mzuri ila bado bustani yako ikaonekana kuwa imepooza.Kinachochangamsha bustani ni urembo na ubunifu unaoonekana katika bustani yako. Jitahidi kubuni  kuotesha maua kwenye vifaa tofauti zaidi ya vyungu vya kuoteshea maua. Nilishatoa makala mengi siku za nyuma yanayoelezea kuhusu ubunifu katika kuotesha maua.

Hebu angalia picha zifuatazo kuona ubunifu  pamoja na urembeshaji wa bustani.