Skip to main content

KERO:MTEGEMEA CHA NDUGU HUFA MASIKINI

Kuna familia za ajabu kweli humu duniani. Utakuta mmezaliwa watoto kadhaa katika familia yenu na wote mmekuwa na maisha yenu na mna familia zenu. Sasa kuna ambao mbali na kuwa na familia zao, hutaka kuwatumia wenzao kama vitega uchumi.Wao hujali maisha yao na ya watoto wao tu na hufanya lolote ili matakwa yao yafanikiwe. Mfano ,kama wanakuona una unafuu wa maisha (wakati mwingine siyo hivyo, wanakuona hivyo kutokana na msaada ulionao aidha kutoka kwa mke/mume) basi watajaribu kukuhadaa katika kila kitu hususan wakijua una shauku ya kujenga, kununua kiwanja n.k.Kinachotokea hapa hutapata kiwanja wala nini.Pesa zako zitatumika zote maana familia yote imetolea macho pesa hizohizo au wote wamejikusanya katika biashara ndogo ya familia ambayo kwa mtu mwenye akili timamu ukiangalia unaona kabisa hakuna kinachoendelea hapo zaidi ya watu kwenda kupunga upepo na kurudi nyumbani.Ndiyo hapo watakapokuua kwa shinikizo la damu pale utakapodai pesa zako!Kwani utapigwa stori zisizoeleweka au watafanya kila wawezalo kuhakikisha huendi katika eneo la tukio. Tujifunze kuwa si ndugu wote wana nia nzuri kwetu,Kikubwa angalia familia uliyonayo yaani mke/mume na watoto kwanza, na hapa ndiyo utapata maendeleo.Jaribu kutumia akili yako mwenyewe na si kuburuzwa.Shirikiana kimawazo na mke/mume wako zaidi ili kufikia malengo vinginevyo unastaafu ukiwa huna hata kibanda wala kiwanja ila una mipango yako hewa isiyokamilika! Anaesikia na asikie.

Tuache kutumiana,tutafute kwa jasho letu.

Asante mdau uliyetuletea kero hii.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.MICHORO MBALIMBALI YA HINA

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA