Skip to main content

INGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE?

Jumanne ya wiki hii imetokea kama bongo movie, ishu ilikuwa hivi:-

Nina rafiki yangu ambaye tulisoma chuo program moja Coet na ku graduate pamoja. Mwanzoni alikuwa na kazi yake kampuni moja hivi hapa mjini na mie nilikuwa na Kampuni nyingine.

Katika kubadili kazi tulikutana kwenye interview kampuni moja Msasani na kwa bahati nzuri mie na yeye tukafanikiwa kupata nafasi na June mwaka huu tukaanza mzigo na hiyo kampuni.

Juzi tukiwa Ofisini akaniaga anaenda EPZA kwa wakala wa Fedex kuna mzigo alikuwa anautuma USA. Akaacha laptop yake akiwa anajua anaenda na kurudi, foleni na kuprocess mzigo ikachukua muda kidogo.

Akaamua asirudi ofisini akanipigia nimchukulie laptop yake then nimpitishie Mabibo mwisho kwani ana mgeni wake anamsubiri pale na mimi hiyo ndo njia yangu ya kila siku.

Muda wa kazi ulivyoisha nikaondoka mdogo mdogo nikijisogeza Mabibo Mwisho, nikiwa Bigbrother akanipigia kuwa yupo Muleba Bar na mgeni wake so niende direct hapo. Kufika pale nikatafuta parking ila sehem niliyopark sikuwa na amani kabisa, wakati huo workmate amenifuata na kunambia nipark kisha niende.

Kuna gari ikawa inatoka so nikawa naisubiri itoke mie ndo niweke hapo nikajikuta nipo nje pale kama dakika kumi hivi.Nyuma ya pazia nina 'demu' anaishi Mabibo Mwisho na asubuhi nilikuwa nimeongea nae anasema anaumwa.

Nikamwambia jioni ntapitia kumuangalia. Nikawa nawaza kwa kuwa na laptop ya workmate basi nikashakuwa nimekaa chini na kutulia nimpigie kuwa niko Mabibo Mwisho Muleba Bar aje.

Duuuuh naingia pale mgeni wa jamaa ndo dem wangu, Workmate akaanza kutambulisha lakini dem akadakia na kusema tunajuana. workamate kauliza mnajuana vipi na wapi?

Mie nikazuga na kupotezea nikiomba huduma ya kula na vinywaji kwani nilikuwa na njaa sana. Nikaagiza Castle lager baridi nikapiga fasta kama maji, mara dem anasema mie na roho mbaya mbona sijaenda kumuona?

Akanisms kuwa workmate ni rafiki yake tu meanwhile akamtumia sms workmate akimwambia mie ni rafiki yake pia. Nikaona ili nisiharibu theme yao nikapiga castle lager tatu fasta nikalipa bill yangu nikasepa waendelee ku enjoy ili nisiharibu mood yao'Sijafika mbali sms inaingia eti "Umeninunia?, huyu ni rafiki angu tu". sikujibu kitu nikauchuna mpaka leo sijamuuliza kitu, sasa anajishtukia pande zote mbili kwangu na workmate.

Kama Bongo Muvi vile, ungekuwa wewe ungefanya nini kwa 'demu' huyu.
CHANZO: jamii forums

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.