Monday, 14 September 2015

BAADHI YA MIJENGO YA WATU WANAOJITAMBUA JIJINI TANGA

Inafurahisha kuona watu wanafanya vitu  vya maendeleo namna hii.Huku ndiyo tunaita kujitambua.Kuna wengi wetu hatujitambui kabisa.Maisha ni mapambano hivyo unatakiwa kufikiri kesho utakuwa wapi na utaishi vipi.Wengi wetu tunaishi kwa kutazama leo tu.Hatushauriki au pengine hatutaki ushauri kwa vile tunajiona kuwa tunajua kila kitu.Tunaendekeza anasa zisizo na maana huku hata viwanja hatuna.Kuna watu wanaanza maisha kila siku bila ya kuangalia au kujali umri.Mtu akiwa na gari anaona kwake ndiyo maisha. Hii yote ni kuendekeza anasa hususan uzinzi.Watu wengi wanafeli maisha kwa kutokujua nini wanahitaji maishani mwao. Hii hupelekea wengi wao kufa maskini.Wengi wanadhani maisha ni kufurahia tendo la ndoa tu kumbe kuna zaidi ya hapo.Siku zote katika maisha mthamini yule aliyekuthamini ukiwa na hali duni.Huwezi kuchumia juani na mwenza wako halafu wakati wa kula kivulini unamkana na kula na mwingine. Utakapokuja kumkosea huyu iwe ni mke au mume basi jua maisha yako ya raha yamefikia ukingoni kwani mkono wa Mungu hautakuacha.Huna utakachofanya kikafanikiwa MILELE na utachekwa na jamii kwa kuonekana ``LOOSER``
TAFAKARI NA CHUKUA HATUA!