Skip to main content

STATUS ZENU ZA WHATSAPP BADILISHENI SASA


imagewwsKuna rafiki zangu wa WhatsApp wwananichekesha sana na status zao;.
 1. Mtu ameandika “Sleeping” , sasa leo siku ya tano, si kishakufa huyu?
 2. Mwingine kaandika “Driving” toka mwaka jana Agosti, naona atakuwa anakaribia Afghanistan saa hizi
 3. Haya jamaa najua kalazwa anaumwa lakini kaandika “Happy” we vipi ndugu yangu?
 4. Huyu mdada kaandika “Available”. Sijui anajua maana yake? Tukikuibukia utaanza mitusi
 5. Mbosi huyu hajabadilisha status mwaka wa pili sasa, “Hey there! I’m using

WhatsApp” sasa unadhani sijui? Tungekutanaje kama hutumii Whatsapp?
 1. Superstar wetu mmoja kaandika “Urgent calls only”. We vipi? Kwani we faya, au ambulens au polisi?
 2. Haka kabishoo kameandika “Can’t talk, WhatsApp only”. Sasa una simu ya nini? Si uitupe uwe unashinda Facebook? Simu kazi yake ya kwanza kuongea sio Whatsapp, pambafu we.
 3. Huyu mshamba kaandika “At the movies” wiki ya saba sasa, sinema gani ndefu hivyo wewe? Au unafanya kazi ya kuuza tiketi hapo sinema?
 4. Dogo kaandika “At school” sasa Whatsapp ya nini? Utapata Div O wewe
 5. Mwezi wa pili sasa mchepuko umeandika “Busy” hivi busy unafanya nini? Nikiacha kukutumia credit utaanza kelele
 6. Hahahahahaha eti “Battery about to die” miezi sita mfululizo, badilisha hiyo betri? Au mtaa wenu hakuna umeme miezi sita hujachaji simu? Si kalalamikeni TANESCO? Au nikununulie jenereta? Unaudhi
 7. Hivi najiuliza we mdada huu mwezi wa nne sasa eti “At the gym” unajitayarisha kwa Olympic
 8. Bosi status yako ya “In a meeting”  mwezi mzima inachekesha, maliza huo mkutano rudi kwenu. Kubwa zima jinga
WAHUSIKA BADILISHENI KABLA SIJAWABLOCK

CHANZO: John kitime

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.