Nilipokuwa jijini Tanga hivi karibuni nilibahatika kutembelea
kituo cha watoto kijulikanacho kama COLLEGINE SISTERS OF HOLY FAMILY ORPHANAGE (Nyumba
ya furaha).Kituo hiki kipo karibu na ilipokuwa Plaza Inn.Katika safari hii
ambayo ilikuwa ni ya kifamilia tuliambatana mimi na ndugu zangu.
Kabla ya kwenda kituoni hapo,tuliwasiliana na masista walezi
wa kituo hicho ili kujua mahitaji halisi kwa watoto hao kwani tulidhani ni
vizuri kufanya hivyo kuliko kupeleka tu vitu hata visivyo na ulazima.
Hii tulifanya vizuri sana kwani tuliweza kugundua kuwa kuna
watoto wachanga kabisa ambao walikuwa na mahitaji zaidi.
Siku moja kabla ya kwenda kituoni hapo tulinunua mahitaji kama
walivyotaka.Siku hii kulikuwa na mvua kubwa ila haikutuzuia kufanya manunuzi.
Tulinunua maziwa, lactogen 1 & 2, pampers na juice. Hivi ndiyo vitu
walivyotaka tuwapelekee.
Mtoto mdogo kuliko wote, Sophia, miezi mitano (5).Aliokotwa akiwa na siku 3 baada ya kuzaliwa
Mtoto George mwenye umri wa miezi 7
Bonyeza READ MORE kusoma habari yote na kuona picha zaidi
Tulikwenda kituoni hapo siku ya jumamosi tukiwa watu watano
(5).Kati ya hawa watu mmoja alikuwa ni mtoto wa miaka 14. Huyu ni mtoto wa kaka
yangu.Tulimchukua kama njia ya kumfanya anapokua ajue kuwa jukumu la kusaidia
wenye mahitaji ni la jamii yote akiwemo yeye.
Kituoni hapo tulipokelewa vizuri na masista pamoja na
watoto.Sista aliyekuwa na sisi katika tukio hilo ni sista Marcelina.Sista
Marcelina alitueleza historia ya kituo kwa ufupi.
Kituo kilianzishwa mwaka 2006 kikiwa na watoto 14 tu. Kwasasa
kituo kina watoto 54 wa umri tofauti. Mtoto mdogo kabisa, Sophia, ana miezi
mitano(5).Na mwingine, Georgr, ana miezi saba (7).
Watoto wa kituoni hapo wanasoma shule mbali mbali zilizopo
Tanga mjini na sehemu nyingine. Kuna watoto ambao wamemaliza sekondari na
wanafanyakazi na kuna wengine wapo vyuoni.
Katika kusaidiana ulezi, watoto wenye umri mkubwa husaidia
kuwaangalia wadogo zao.Kwa kweli ni hali ambayo inagusa sana kwa
uhalisia.Kikubwa na chenye kutia faraja, watoto wote wana furaha sana.Walifuahi
sana kutuona na tukaongea pamoja na kucheza nao huku wakapiga picha nyingi na
sisi.
Kituo kilianzia katika nyumba hii
Kituo hiki kilianza na nyumba ndogo ya kawaida ya kuishi na
kwa jinsi siku zilivyokwenda na idadi ya watoto kuongezeka nyumba ilikuwa ndogo
hivyo kupelekea kuanza kujenga jengo lingine la ghorofa 2 pembeni.Ujenzi wa jengo
hilo unaendelea bado na unafanikishwa kutokana na michango ya wadau mbalimbali.
Jengo jipya la kituo
Ningependa kutoa wito na kuwaomba wale wote wenye mapenzi mema
wawasaidie watoto hawa kwani kutoa ni moyo na si utajiri. Kumbuka kila kidogo
utakachopeleka kitabadilisha maisha ya watoto hawa na Mungu atajaza pale
ulipopunguza. Badala ya kutumia pesa kwa kunywa pombe au kuhonga ni bora
ukawasaidia watoto hawa upate Baraka za Mungu.
Watoto bado wana mahitaji mengi ikiwemo chakula, nguo n.k.Vilevile
jingo lao linahitaji kukamilika.
Nitaweka namba ya sister Marcelina hapa kwa wale wanaotaka
kusaidia watoto hawa.
Watoto wakubwa wanasaidia kulea wadogo zao
Watoto wakiwa na nyuso za furaha
Watoto wakiwa kituoni
Jengo jipya la kituo
Lactogen 1 & 2 tulizopeleka
Juice tulizopeleka
Tukiwa na sister Marcelina na watoto
Sister Marcelina kulia akiwa na watoto pamoja na ujumbe wetu
Tukiwa na watoto
Mtoto huyu aliyepakatwa na kaka yangu, alimng´ang´ania hakukubali
aliporudishwa kwa sister
Mtoto George, mwenye umri wa miezi 7, akiwa amelala baada
ya kubembelezwa
Tukisaini ofisini
Mtoto wa miaka 14, Kelvin,ambaye tulifatana nae,
akifurahi na mtoto
Tukiwa na baadhi ya watoto na sister Marcelina
Tulifarijika sana na safari hii. Asante nyingi kwa sister Marcelina na wahudumu wote wa kituo hiki.
MNAWEZA KUWASILIANA NA SISTER MARCELINA KWA NAMBA: 0765 565 007
No comments:
Post a Comment