Friday 9 October 2015

JE, UNATUMIA GESI KUPIKIA? SOMA HAPA




Je unatumia gas kwa kupikia?
Tafdhali soma ujumbe huu na uchukue tahadhari ili isitokee kwako. Hili linaweza kuwa ni kosa la kawaida katika kila nyumba.

JINSI ILIVYOTOKEA.
Jiko la gas lilikuwa linawaka na mapishi yakiendelea.
mama akaona mende jirani na sinki la kuoshea vyombo. Mara akachukua kopo la dawa ya mbu na kupuliza karibu na lile jiko la gas linalowaka.
Ulitoka mlipuko mkubwa na ndani ya muda mfupi yule mama alikuwa ameungua kwa asilimia 65.
Mumewe alikimbilia kuuzima ule moto na nguo zake nazo zilishika moto.
Mumewe bado yuko hospitali akiuguza majeraha ya moto na bado hana habari kwamba mke wake alifariki alipofikishwa tu hospitali.
Ni vema tukafahamu kuwa dawa zote za kuulia wadudu "Hit", "Marten", "heaven", "Raid" "rungu" n.k. zina mchanganyiko wa madawa mengi yanayosababisha mlipuko mkubwa.
Mchanganyiko huu wa madawa ni rahisi sana kusababisha mlipuko haraka sana.
Tafadhali elimisha wanafamilia yako na rafiki zako kuhusu jambo hili na sambaza ujumbe huu.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...