Skip to main content

KERO: USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO!Nimegundua kuwa ni mama pekee ndiye mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae. Mama yako hawezi kukutupa au kukukataa katika namna yeyote labda awe na matatizo ya akili.
Mume au mke anaweza kukugeuka haijalishi mmetoka nae wapi.Kweli sisi binadamu tunasahau haraka mno.Na kitu kibaya tunasahau hata mema ambayo wenzi wetu wametutendea.Mtu anaweza kuamua kumfukuza mwenzi wake kama mbwa na kusahau kabisa uzuri wa hayo maisha anayoishi kwasasa yamechangiwa kiasi kikubwa na huyo anayemfukuza.Watu huacha mazuri yote waliyokuwa nayo kabla ya kukutana na wenza wao na kuamua kuwafuata wenzao hao kutokana na mapenzi.Watu huacha kazi zao nzuri na maisha mazuri waliyokuwa nayo kwaajili ya mapenzi.Watu huuza na kuweka rehani vitu vyao vya thamani kwaajili ya mapenzi. Watu hupoteza wapendwa wao wakati wakilinda penzi ILA mwishoni huyo unayemfanyia hivyo hakumbuki yote haya.Anaacha mbachao kwa msala upitao.

Anapokuwa amepata mwingine hujali kukidhi tamaa zake za mwili, basi.Kama ulimsadia hiyo ilikuwa ni charity tu kwake.Kuna watu wamezoea kuoa na kuacha au kuolewa na kuachwa.Kwao haya ndiyo maisha,Na watu hawa ukiangalia zaidi ya kuwa na nguo za kuvaa hawana asset yoyote. Watapata wapi asset wakati wako busy na kutafuta wanawake/wanaume wapya kila siku ili kukidhi tu tamaa za mwili?Mtu anazeeka hana chochote na bado ana matumaini kuwa ETI bado ana muda wa kupata mali au kutengeneza maisha yake.Hapa ndipo unapoona maana ya ile methali ``AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE``.
Mpaka unaweza kujiuliza hivi mtu huyu karogwa au ndiyo akili yake?Kwanini mtu huna wivu wa maendeleo? Je, na wewe ni mmoja wao?

TAFAKARI NA CHUKUA HATUA.

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.