Skip to main content

MOTHER AND DAUGHTER LOVE!

Katika safari ya maisha mtu ambaye hawezi kukukana na atakayekuwa na wewe siku zote,katika shida na raha ni MAMA YAKO TU.
Kwa mama anaejitambua,mtoto wake ndiyo kila kitu kwake.
Siku zote mama humtakia mwanae mafanikio na huumizwa na tatizo litakalompata mwanae.Mama ndiye pekee  anayeweza kukusikiliza na kuamini unachosema.Mama ndiye anajua tabia halisi ya mwanae.Mama anajua udhaifu na ushupavu wa mwanae.
Mama ndiye unayeweza kumweleza matatizo yako akakusikiliza na kukusaidia kwa uwezo wake.Kwanini?Kwa sababu unapoumia wewe na yeye huumia pia.
Baba anaweza kumwacha mama yako na akaenda kutafuta mwanamke mwingine.Ila mama wengi ni wagumu kuwacha watoto wao walelewe na watu wengine.Kwanini?Kwa kuhofia kuwa mama wa kambo au mtu mwingine hataweza kumpa mtoto wake mapenzi halisi ya mama.Ingawa si mama wa kambo wote ambao wana roho mbaya.
Tuwaheshimu mama wote wanaojitambua.
NANI KAMA MAMA.

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.