JARIBU KUSOMA STORI HII MPAKA MWISHO NA UTAJIFUNZA KITU
“Nilipofika
nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia,
Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa
tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa.
Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi
nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka
kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno
yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake.
Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si
mwanamume!’ Usiku ule,hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi.
Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa
hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali
kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo
yote yalikuwa kwa Mary. Kwa kweli nilimdharau mke
wangu!
Huku
moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha
kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya
kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.
Mke
ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea
huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma
kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa
sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia.
Kwangu
mimi kilio chake kilinipa nafuu. Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa
majuma
kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi. Siku
iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika
jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa
moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka
baada ya kula raha za kufa mtu na Mary.
Usiku
nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa
nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka
yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi
mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha
mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa
kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa
kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda
mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo
kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba
nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu.
Akaniomba
na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka
kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa
kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na
masharti yake ya ajabu. Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na mke
wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hataakitumia ujanja wa namna gani
talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa
dharau. Mimi na mke wanguhatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki.
Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi
sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’.
Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi
sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke
wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu
juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka
chini nje ya nyumba.
Alienda
kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini
kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu.
Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua
kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa
binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa
yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.
Siku
ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke
aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita
ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu
jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na
zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha
zaidi.
Alikuwa
akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa.
Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu
amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma...
mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa
chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende
kazini’.
Kwake
kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu
alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu.
Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha
nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni.
Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia
mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake
ulinitia mashaka.
Siku
ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu
alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha
yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini.
Nikashuka
garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza
kubadili nilichoamua.Nikapand ngazi. Mary alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani,
Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’.
Akaniangalia
kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa
mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki kumtaliki mke
wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa
maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani.
Nimetambua
hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha
yetu,
nampenda
mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’ Ikawa
kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza
mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka
la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza
aandike nini kwenye kadi.
Nikatabasamu
na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo
kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu
kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu
kitandani.
Kumbe
mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa
kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa
karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha
talaka mapema.
Angalau
machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema.
Wengi wanapopata michepuko huchukua maamuzi ambayo huja
kuyajutia baadae. Fikiri kabla ya kutenda kwani Majuto ni mjukuu. Usije
kupoteza kabisa dira ya maisha yako. Utamaliza
bucha kwa nyama ileile.
No comments:
Post a Comment