Monday, 16 November 2015

NIMEPENDA HII KUTOKA KWA DINA MARIOS


Dina Marios
Maisha haya kila mmoja anasafari yake namna atakavyo anza na namna atakamaliza ni Mungu ndio anajua.Kwa mfano kuna mtu atamaliza chuo akiwa na miaka 20 ata struggle kwa miaka 5 kupata kazi.Mwingine atamaliza akiwa na miaka 25 na akapata kazi mapema tu baada ya kumaliza chuo.Mwingine anaweza kuolewa bikira na kusubiri miaka 10 kupata mtoto..mwanamke mwingine alotoa mimba kibao huko nyuma anaolewa na kushika ujauzito hapo hapo.Jamaa mmoja anakuwa MD katika kampuni akiwa na miaka 38 na kufariki akiwa na miaka 56,jamaa mwingine anakuwa MD akiwa na miaka 50 na anaishi mpaka miaka 90.

Maisha ni nini?maisha yana kona nyingi,mkanganyiko,ups and down,suprises na disapointments.
Maisha humpa kila mmoja wetu nafasi mbali mbali na nafasi hiyo ikipotea inaweza isirudi tena na ikirudi ni kwa huruma ya Mungu.
Ni juu yetu sisi kuwa na subira,kujiandaa,kuitambua na kuipokea hiyo nafasi/fursa.Kila siku tunajifunza njiani hakuna alobarikiwa yote au mwenye kujua yote.Kuna sababu katika kuanguka na kupigika. Tunapoanguka hatuanguki wote hii ni kwa sababu nikiwa chini nimeanguka,nipo mnyonge na sina matumani...wewe ulie imara uninyanyue na kunifariji,kunipa moyo na matumaini mapya.

Mungu hakutuahidi kuwa maisha yatakuwa rahisi ila ametuahidi hatatuacha tuaibike.Japo kuwa maisha hayatabiriki tujifunze kuwa wanyenyekevu na kuamini Mungu anayafanyia kazi yoote yatusumbuayo japo hatuwezi kuona kwa sasa.
Mtihani wowote,jaribu lolote,anguko lolote,masikitiko,huzuni vitapita siku moja.Ipo siku Utasimama imara tena,utacheka tena na haya yote wakati yakitokea na wewe utamuinua na kumpa matumaini mtu aliyepoteza matumaini kwa wakati huo.Na mtu anapopatwa na majanga usicheke wala kufurahia ukasema afadhali.Yeye anaepatwa na jaribu ipo siku atainuka na wewe utakuwa chini ukilia yamekufika.
Never loose hope kuwa na imani ipo siku tutayasimulia tu kuwa ni mapito katika safari hii ya maisha.



No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...