Tuesday, 8 December 2015

JIHADHARI NA NDUMILAKUWILI

Ni mtu/rafiki anaye jifanya mwema na kukupenda mkiwa pamoja, ukipa mgongo anakusema vibaya kwa watu na kufanya jambo lolote ili akuharibie. Ndumila kuwili siku zote wanakuwa ni watu wa karibu marafiki, jirani, ndugu, mfanyakazi mwenzio, ndio maana hata siku moja hukai ukawaza anaweza kuja kukutenda. Kitu kikubwa chukua tahadhari mapema;

Kaa mbali na mtu anayependa kuhadithia au kutoa siri za watu wengine, ujue siku akija kujua na ya kwako ataenda tu kuyatangaza. Na ukiwa unapenda kumsikiliza mtu mmbea, anaweza hata kukugeuzia kibao kwa watu kuwa umewasema wakati yeye ndiye aliyesema.

Usipende kuongea mambo yako kwa kila mtu, hata kama ni mafanikio, ujue ndumila kuwili wengi wana chuki, wivu hawapendi kuona wengine wana fanikiwa, akijua mambo yako yanaenda vizuri atafanya kila analo weza uharibikiwe iwe kazini, ndoa, heshima yako kwa watu nk.

Ndumila kuwili akishakutenda usipende kumwamini tena, mwingine anaweza kupamba msamaha lakini moyoni hajamaanisha, rafiki unaweza kununua urafiki ila mwingine ni nduguyo, mfanyakazi mwenzio lazima kuna mahala utakutana naye, ila kwa vile nyoka umeshamjua unachukua tahadhari mapema.

Ndumila kuwili akishakutenda mpe ukweli wake, uguza maumivu mwombe Mungu akusaide endelea na maisha yako, haina haja kukaa unaendelea kumtumia meseji au kumpigia simu mnatukanana mpaka kwenye mitandao , inauma ndio lakini muhimu ushajifunza na yaliyotokea.