Wednesday, 2 December 2015

KILA KIUMBE WA KIKE- CHRIS MAUKI


Wanaume wenzangu tuelewe na pia hili lituingie akilini kwamba sisi na wake zetu tumeumbwa tofauti sana. Kila mwanamke ndani ya moyo wake na nafsi yake kuna kiu isiyo na msimu. Kiu iliayo kwa sauti ikitamani kudekezwa, kupendwa, kujaliwa na kuangaliwa kwa upendo kama mtoto mdogo. Sasa wewe leo mwenzako anadeka kidogo unamkurupusha kama mwizi eti "acha utoto weweee, unamdekea nani sasa" nani kakwambia mapenzi yana kukua, au yana ukubwa na udogo? Usiishi na mke wako kama mwanaume mwenzako, usimfanye yeye kama kifaa, yeye sio trekta au jiko au kompyuta au sufuria. Yeye ni kiumbe mwenye hisia tena kali tofauti kabisa na wewe. Kama haujafundishwa basi kamuulize mama yako atakwambia, na kama atakwambia tofauti basi mlaumu baba yako kwa kumfanya mama yako akawa kama wewe unavyomfanya mke wako leo. Pokea hiyo kwa leo - Chris Mauki