Monday, 21 March 2016

JIKONI KWANGU: SUPU YA KUKU NA MBOGAMBOGA (CHICKEN VEGETABLE SOUP) MAHITAJI
250g Steki ya kidari cha kuku(chicken fillet)
1 Hoho ndogo ya kijani
1 Hoho ndogo nyekundu
2 viazi ukubwa wa kati
1 karoti kubwa
1 kitunguu maji ukubwa wa kati
3 decilita krimu ya maziwa/ maziwa
¼ kijiko cha chai pilipilimanga
1 leek
¾ kikombe njegere
1 cube chicken stock
2 Lita maji
1 kijiko cha chai
3 vijiko vya chakula Unga wa ngano/unga mlaini wa mahindi
Chumvi(kiasi unachopenda)
FANYA HIVI
Katakata kuku katika vipande vya ukubwa wa 1 cm
Katakata mbogamboga zote katika vipande vya ukubwa wa 1cm kasoro leek ambayo mimi huikata katika duara(slices)
Tumbukiza vipande vya kuku, vipande vya mbogamboga, njegere, na chicken stock cube katika sufuria. Weka lita 1 ya majina bandika jikoni. Acha supu yako ichemke na kuiva katika moto wa wastani. Maji yakikauka,ongeza lita 1 iliyobakia.
Chukua kibakuli kidogo na weka unga wa ngano. Weka maji kiasi katika unga kutengeneza uji mwepesi.
Weka mchanganyika huu wa unga wa ngano katika supu inayochemka.Unga wa ngano utafanya supu yako iwe nzito kidogo.
Weka pilipili manga, binzari na chumvi kuweka ladha.
Weka krimu ya maziwa/maziwa na koroga ili kuzuia supu isiungue.(Unaweza kutokuweka krimu/maziwa kama hupendelei)
Supu ipo tayari na inawezwa kuliwa na mkate,chapati au hata yenyewe.
Mimi hula yenyewe tu na ninashiba kabisa.
NB: Unga mlaini wamahindi kama unaupata ni mzuri zaidi maana hautoi mabonge kama unga wa ngano vinginevyo tumia tu unga wa ngano ila changanya vizuri ili kuepuka mabonge!