Monday, 20 June 2016

NDUGU CHANZO CHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA

Katika ndoa nyingi za Kiafrika; wanandoa huingia na msururu wa watu kwenye ndoa. Unakuta mke, mme ama wote wawili wana watu wanaowategemea, (extended family). Hawa watu wanaomtegemea mwenzi, kuna saa huwa ni chanzo cha migogoro katika ndoa. Kuna wanaotegemea kusomeshwa, wengine kulishwa, kuvikwa n.k. Mtegemewa akikwama kutimiliza mahitaji yao wanaanza maneno, visa, vitimbi n.k. Sana sana upande wa ndugu wa kiume ndiko huwa kuna shida zaidi. Ndugu wa kiume wakiona hawapati yote wanayotaka huwa wanainua vita dhidi ya mke (yaani wifi, shemeji na mkamwana wao); wakiamini kuwa ndie anaemzuia mumewe (kaka yao, kijana wao, ndugu yao) kuwasaidia. Ni vema wanandoa kufahamu mambo manne kuhusu hili: 1) Ndoa ni taasisi inayojitegemea na haitakiwi kuyumbishwa na matakwa ya wengine hata kama ni wazazi, mawifi, mashemeji n.k 2) Hata kama ukiwa/mkiwa na huruma kiasi gani hamuwezi kumsaidia kila anaekuja kutaka msaada na hata mkisema msaidie kila mtu hamuwezi kuwaridhisha wote. Maneno na lawama vitakuwepo tu. Kwa hiyo, kama wanandoa lazima mkae chini kwa pamoja mkubaliane ni watu gani wana ulazima wa kuwasaidia kutoka pande zote mbili(kikeni na kiumeni), kisha mnawasaidia kwa kadiri ya uwezo mlionao. Wengine acheni tu wawalaumu kwa maana lawama haziui! 3) Msijichoshe kuwasaidia ndugu kupita uwezo wenu, kumbukeni na ninyi ni familia mnahitaji pia maendeleo katika ndoa, mkiruhusu watu "wachotage tu", mtakwama halafu hao hao waliokuwa wanachota watageuka kuwasema 4) Katika wale mliokubaliana kuwasaidia tumieni mfumo wa kuwawezesha wajitegemee badala ya kuwapa kila siku. Wanaowezekana kusoma wasomesheni hata kozi tu ili wajitegemee, waliokataa shule watafutieni hata mitaji. Badala ya kutuma fedha kila mwezi kwa wazazi kule kijijini fanyeni ubunifu muwaanzishie japo miradi midogo midogo kama kufuga kuku, ngo'ombe, n.k. MWISHO: Katika wale mnaowasaidia msilee uzembe, kama mtu mnamsomesha lakini anakula ada ama kufanya uhuni, msimchekee! Kama mnampa mitaji lakini anashinda akiipoteza; msimvumilie. Kuna baadhi ya extendend family members ambao ili NDOA IWE NA USALAMA, ni lazima kufanya maamuzi magumu dhidi yao. Vinginevyo mnaweza kuvunja ndoa kwa kukumbatia ndugu wenye miiba miilini mwao(wasiobebeka).
CHANZO:Ni wakati wako wa kung'aa on facebook

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...