Thursday, 16 June 2016

NUKUU YA LEO:TUSILIPE WEMA KWA UBAYA

Tuepuka kulipa ubaya kwa aliyekufanyia mema.Utakuwa na furaha ya muda mfupi sana (kama utakuwa nayo).
Hii ndiyo KARMA.Utapata mema kama ukitenda mema na yatakupata mabaya zaidi ya uliyotenda ukitenda mabaya.
Tumeona wengi wameharibu kabisa mwelekeo wa maisha yao eidha kwa tamaa ya kupata zaidi au kwa ujinga tu.
Wa kujenga au kuharibu maisha yako ni wewe mwenyewe kutokana na matendo yako.Tuepuke kuumiza wengine kwa  kudhani tunajitengenezea au ndiyo tunakaribisha PEPO katika maisha yetu.Kumbe  ndiyo tunakaribisha ghadhabu ya Mungu.Hapa ndiyo mwanzo wa majanga kudhallilika na kufedheheka. Kwani ulichokifanya ni sawa na kukata tawi la mti ulilokalia  mwenyewe.Ni wewe ndiye utaanguka na si uliyemtendea mabaya.
Tuangalie matendo yetu kwa wengine!

SIKU NJEMA