Thursday 8 September 2016

KERO:HIVI NI HAKI KUTUMIKA NA NDUGU WA MUME/MKE?

Ni ukweli usiopingika.Kuna watu wanaishi kwa kutegemea wengine.Wao kama wao hawataki kujishughulisha na chochote.Mtu anasubiri kula yake,kuvaa yake n.k aletewe na mtu mwingine.Hivi huyu anaekuletea yeye anapewa na nani?
Binafsi sikubaliani na hili.

Hii sana hufanywa na wale wenye ndugu zao waliopo ughaibuni .Wengi wao hawajui ndugu zao huko ughaibuni wanaishi vipi.Ukweli ni kwamba si kila aishiye Ughaibuni amefanikiwa kimaisha.Wengi wao aidha hawana kazi kabisa au hawana kazi za kueleweka.

Tatizo kubwa lingine ni UVIVU .Wengi wao ni wavivu na wanachagua kazi za kufanya.
Wengi akishalipa Ankara za mwezi, chakula na madeni habaki na kitu.
Kwa wale wenye kujituma ndiyo hufanikiwa.
Mbaya kama ndugu yenu ameona au kuolewa basi lawama zote mnazielekeza kwa mke/mume kama wao ndiyo chanzo cha nyie kutopewa msaada. Ni aibu isiyoelezeka kwa kweli kwa wale waishio maisha haya.Mtafitinisha mpaka mvuruge mahusiano.

Mtashawishi ndugu zenu kuoa/kuolewa hata mara 100 ila tatizo litakuwa lipo palepale kwani hamjatibu tatizo zaidi mnaongeza.Umri pia hausubiri hayo mabadiliko yenu. Mwisho ni kuharibu maisha ya mwenzenu huku mkijiweka pembeni bila kumsaidia.

Jamani,waelezeni ndugu zenu ukweli wa maisha mnayoishi maana kwa kutokufanya hivyo maisha yenu yataharibiwa na hao hao ndugu zenu.

Hivi katika dunia ya leo ni haki kweli mtu kuishi kwa utaratibu huu?
TAHADHARI KISHA CHUKUA HATUA!!

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...