Wasanii kadhaa ambao walikuwa na show week hii wametumia busara na heshima kubwa kuhairisha show zao ili kumpa heshima Marehemu, isingekuwa vema kama watu wangeendelea kufanya yao wakati mwenzao amewatoka.
Baadhi ya wasanii
hao ni Lady Jay Dee ambae alikuwa na show ya kuadhimisha miaka 13 kwenye game
ijumaa hii ya tarehe 31, Mwana Fa na show yake ya The Finest nayo ilitakiwa
kufanyika ijumaa hii tarehe 31, T.I.D ambae alitakiwa kufanya show jana 28
ndani ya Maisha Club na show nyengine Bukoba hivi karibuni, Ben Pol ambae
tarehe 1 June ndio alikuwa anatarajia kuachia video ya nyimbo yake ya Jikubali
nae amehairisha.
Wasanii wengine walioahirisha shows ni pamoja na Kalapina pamoja na Izzo Business.
Wasanii wengine walioahirisha shows ni pamoja na Kalapina pamoja na Izzo Business.
No comments:
Post a Comment