Thursday, 20 June 2013

JE,KILIMO KINAWEZA KUMKOMBOA MTANZANIA?HIVI NI KWELI KUWA WANAWAKE NDIYO WAKULIMA WAKUU?





Wadau,je ni kweli kuwa wanawake ndiyo wakulima wakuu?Je,kilimo chenyewe kinawalipa au wanalima kwa mazoea tu?Je,vifaa vya kilimo wanavyotumia ni vya kisasa au la?Je,wana elimu kuhusu kilimo bora na uhifadhi wa mazao?Je,wana uhakika wa soko?


Kama wanawake ndiyo wanalima zaidi ya wanaume je,wanaume wapo wapi au wanafanya kazi gani?
Tutakapopata majibu ya maswali haya ndiyo tutajua kuwa kilimo kina mapungufu gani na nini kifanyike ili kukipa uhai.Kwa mtazamo wangu kama kungekuwa na mikakati mizuri katika kilimo,vijana wengi wasingekimbilia mijini na badala yake wangejikita katika kilimo.
Nadhani imefika wakati serikali isimame kwa dhati kuhakikisha kuwa wakulima wadogo wanapatiwa ujuzi wa kilimo na wanatafutiwa masoko ya uhakika ya bidhaa zao.Vilevile wanatumia zana bora za kilimo kama matrekta n,k.Katika masoko tuwavutie zaidi wawekezaji katika viwanda vya kusindika matunda na mboga ili wakulima wetu wawe na uhakika wakuuza mazao yao badala ya kutupa.
Wakulima wanaweza kujiunga katika vikundi na kupewa elimu ya usindikaji(SIDO).Tunaona katika nchi za wenzetu karibu kila kitu kinasindikwa kuanzia matunda mpaka mboga za majani.
Mifano ni kama hii ifuatayo:


Matango
Kwa picha zaidi endelea hapo chini

1 PACKET OF OKRA, LADIES FINGER, VEGETABLE SEEDS

Bamia

 
Spinachi                                                                     Brokoli




Njegere                                                                                                  Uyoga



Kauliflawa                                                                                  sallad



Mchanganyiko wa karoti na njegere.Vilevile kuna mchanyiko wa karoti,njegere na french beans.

french beans

Idadi ya mboga na matunda yanayosindikwa ni kubwa.Kilimo kikitiliwa mkazo sidhani kama kuna atakayetaka kubanana mjini.Kuna bidhaa nyingi za matunda na mbogamboga zinauzwa Ulaya kutokea Kenya na si ajabu nyingine wanakuja kuchukua kwetu katika miji jirani kama Tanga,Arusha na Kilimanjaro.Tuige kwa wenzetu wanafanya nini kwani hatujachelewa.

Imeandikwa na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...