Monday 3 June 2013

KIFO CHA NGWEA SI MTAJI


By Kalunde Jamal, Mwananchi
Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records,P-Funk, ‘Majani’ amewajia juu watu wanaotaka kujinufaisha na msiba wa Albert Mangwair, huku akiwalaani vikali wanaotumia msiba huo kujipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa zisizo sahihi.
 
Majani alisema hayo kufutia kuenea kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha picha ya msanii huyo akiwa amepasuliwa tumbo na kukutwa na pipi za madawa ya kulevya wakati akifanyiwa upasuaji.
Majani amesema kwamba taarifa kwamba alikutwa na pipi za madawa ya kulevya si za kweli kwa kuwa hakuna aliyethibitisha hilo.
“Kuna vitu vingi vya kuwafanya wawe maarufu, lakini siyo kufanya vitu vya kudhalilisha maiti kwani ni maonyo ya dini zote, ina maana watu wamemsahau Mungu kiasi hicho hadi kufanya mambo yasiyoeleweka inashangaza sana, kibaya zaidi kuna baadhi ya watu wapo huko kwa miaka mingi tunawaamini na wao wameingia kwenye mkumbo huo wa kutoa habari zisizo na uhakika,”alisema Majani kwa hasira.
Majani alisisitiza kwamba kuna baadhi ya mambo yanapaswa kuachiwa familia na endapo familia yake itahitaji msaada watoe kadiri wanavyoweza.
Alisema hakuna sababu ya mtu au watu kujinufaisha kwa kifo cha Mangwair ambaye alitumia nusu ya uhai wake kuitangaza nchi kupitia muziki.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...