Saturday 29 June 2013

NMB YAENDELEA KUZINDUA BUSINESS CLUB “SASA NI ZAMU YA KARATU”

P1650255Mhandisi mkuu wa Wilaya ya Karatu, Tulinumpoki Mwakalukwa akitoa shukrani zake kwa NMB mara baada ya kuzindua rasmi  NMB Business Club wilaya ya Karatu. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Karatu , Evarist Mtaro na mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati wa NMB Filbert  Mponzi.
………………………………………………………..
Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.
Katika kulizingatia hili, NMB imezidi kuzindua klabu maalum za wafanyabiashara maarufu kama NMB Business Club. Hadi sasa zaidi ya NMB Business Club 29 zimekwisha zinduliwa nchi nzima.
Kupitia NMB Business Club wajasiliamali wanaowezeshwa na benki ya NMB wamekua wakipata nafasi ya kujifunza jinsi ya  kuandika michanganuo ya biashara zao na pia kuendelea kua vinara wa biashara.
P1650470Mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati wa NMB ,Filbert  Mponzi akimkabidhi mwenyekiti wa  NMB Business Club Paulith Jack  mara tu baada ya kuibuka kidedea kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa NMB Business Club Karatu .
P1650350Sehemu ya wanachama wa NMB Business Club wilaya ya Karatu wakifurahia uzinduzi wa NMB Business Club.
CHANZO:Full shangwe

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...