Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Mtoto
Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar
es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda
mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete
akishuhudia.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo
asubuhi.
asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.(picha na Freddy Maro).
6/27/2013
No comments:
Post a Comment