Thursday 13 June 2013

RAIS JACOB ZUMA WA AFRIKA YA KUSINI AELEZEA MAENDELEO YA AFYA YA MANDELA

ZUMA
Rais  wa  zamani wa Afrika  kusini Nelson  Mandela ameendelea  kubaki  hospitali  kwa  siku  ya  sita  leo  mjini Pretoria . 
Mandela  anaendelea  vizuri  na  matibabu kuanzia  jana  kutokana  na  maambukizi  katika  mapafu, kufuatia siku  chache  ambazo  zilikuwa  za  matatizo kwake.

Rais Jacob Zuma  wa  Afrika  kusini  ameliambia bunge  kuwa  anafuraha  kutokana  na  maendeleo ya  kiafya  ya  kiongozi  huyo  wa  zamani  mwenye  umri wa  miaka  94,  kufuatia  kulazwa  hospitali  siku  ya Jumamosi.
 Zuma amedokeza  kuwa  jana  Jumatano ilikuwa ni siku ya kumbukumbu  ya  miaka  49 tangu  Mandela alipohukumiwa  kifungo  cha  maisha  mwaka  1964.
Amesema  kuwa  fikira za Waafrika kusini  ziko  pamoja na  Mandela  na  familia  yake katika  siku  hii  muhimu  ya kihistoria.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...