Thursday, 13 June 2013

TAMASHA LA FILAMU GRAND MALT KUFANYIKA JIJINI MWANZA JULAI 1-7




 Msanii wa Filamu, nchini, Jaqueline Wolper, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo, wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo (kushoto) ni Mkurugenzi wa Sophia Records walio waandaaji na waasisi wa tamasha hilo, Musa Kissoky.

Na Mwandishi Wetu

TAMASHA la Wazi la Filamu Tanzania maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ mwaka huu linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, wanaamini litafanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mikakati waliyoiweka.

Consolata alisema, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika viwanja hivyo kuanzia Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazoonyeshwa katika kipindi hicho.

“Tumejipanga kufanya uhamasishaji wa kutosha ili kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuweza kuhudhuria tamasha hili. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...