Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2013

MKOA KWA MKOA: LEO TUPO SONGEA MKOANI RUVUMA

Unapozungumzia historia ya Tanzania basi hutaacha kuitaja Songea,ambayo ni makao makuu ya mkoa wa Ruvuma. Songea ndiyo ilikuwa makao makuu ya vita vya majimaji vilivopiganwa kati ya mwaka 1905-1907. Jina la Songea linatokana na kionozi wa Wangoni aliejulikana kwa jina la Songea Mbano. Songea pamoja na viongozi wengine wa Wangoni,walinyongwa na Wajerumani mwaka 1906.
Mbali ya kuwa mkoa wa Ruvuma ni maarufu kwa kilimo hususan mahindi,vilevile kuna utajiri wa mawe a vito aina ya sapphire na ruby.Kwa kumbukumbu zangu binafsi uchimbaji huu umeshamiri katika wilaya ya Tunduru.


Hii ni barabara ya kuelekea Songea
Baada ya Watanzania kukamatwa na dawa za kulevya, hiki ndio kimemkuta Madee akiingia Afrika Kusini

Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.

MWAKYEMBE AVUTIA PUMZI `UNGA` AIRPORT

Kufuatia matukio mfululizo ya kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya wanaodaiwa kuwa ni Watanzania kwenye viwanja vya ndege nje ya nchi wakipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema atalishughulikia suala hilo kama alivyofanya bandarini.
Dk. Mwakyembe ambaye wizara yake ndiyo yenye dhamana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo maalumu na NIPASHE kuhusu ufuatiliaji wa vitendo hivyo vinavyoharibu taswira ya nchi kimataifa.

`MEMORY CARD`YALETA HOFU WAKAZI BUTIAMA

Aina mpya ya ukatili wa kijinsia maarufu kama `memory card' unaohusisha wanawake kuuawa na kunyofolewa sehemu za siri, imezua hofu miongoni mwa wakazi wa wilaya Butiama mkoani Mara.
Kati ya kipindi cha Desemba mwaka jana na Julai, mwaka huu, jumla ya wanawake 14 wanasadikiwa kufanyiwa ukatili huo.
Ukatili huo umebainishwa na wanawake mbalimbali walipokuwa wakizungumza kwenye mdahalo wa kupinga ukatili wa wanawake na watoto wa kike uliofanyika katika kijiji cha Bisumwa, Wilaya ya Butiama mkoani Mara ambapo walisema mauaji hayo yanaongozwa na kundi la watu wanaojiita makhirikhiri.

KATUNI YA LEO

SERIKALI YAWAACHIA WANANCHI KUHUSU MAFUTA YA UBUYU

Mafuta ya ubuyu  Dar es Salaam. Serikali imesema suala la matumizi ya mafuta ya ubuyu sasa inawaachiwa wananchi wenyewe kutumia ama kuacha. Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alisema hayo jana alipotoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa mafunzo ya wataalamu kutoka vitengo vya mbalimbali vya Udhibiti Dawa na Chakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu kutoka nchi 16 za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu. Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu. Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo. Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

MBONI AANGUA KILIO MBELE YA MZEE RUKSA

Na Mwandishi Wetu
HOSTI wa Kipindi cha ‘The Mboni Show‘ kinachorushwa kupitia Kituo cha Runinga cha EATV,  Mboni Masimba Jumapili iliyopita aliangua kilio mbele ya Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipokuwa kwenye hafla ya kufuturisha kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Mtangazaji huyo alimwaga machozi wakati akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na kutoa shukrani zake kwa wote waliomsaidia kufanikisha shughuli hiyo.
Baada ya kutoa shukrani alionekana kuwa mwenye furaha kwa kumtambulisha baba yake mzazi, mzee Masimba ambaye hajulikani kwa watu kama ilivyo kwa mama yake.

MAPENZI YAUA

Hamida Hassan na Haruni Sanchawa
WAKATI Waislamu wakiwa ndani ya Mfungo wa Ramadhani, mapenzi yamemuua kijana Ibrahim Ibrahim ‘Ibra’ wa Kundi la Wakali Danta la Magomeni jijini Dar kwa kuchomwa visu. Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Ibra. Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 27, mwaka huu maeneo ya Magomeni Kagera ambapo ndugu wa Ibra, Ally Jumanne Sanane alidai kuwa, Ibra alichomwa kisu na kijana aliyefahamika kwa jina la Kelvin wakimgombea demu aitwaye Fatma Kiduku.
Mtoa habari huyo alidai: “Fatuma alikuwa ni mchumba wa Ibra lakini pia inaonekana alikuwa akitoka na Kelvin.

Askari kituo cha Osterbay wakamatwa na meno ya tembo 70

WATU tisa, wawili kati yao wakiwa ni askari wa Jeshi la Polisi kituo cha Osterbay jijini Dar esalaam wamekamatwa wilayani Kisarawe Mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha meno ya tembo (ndovu) 70 sawa na kilo 305 kinyume na sheria. Meno hayo ya tembo kwa mahesabu ya kawaida ni sawa na Tembo 35 ndiyo wameuawa na kwamba thamani ya meno hayo ni  zaidi ya sh, milioni 850 fedha za kitanzania.

IRENE UWOYA KUTOKA KIVINGINE NA SHOW YAKE YA KUTENGENEZA NA KUKARABATI NYUMBA ITAKAYO RUSHWA CLOUDS TV

Irene Uwoya anakuja na kipindi chake kipya cha Tv kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati  nyumba mbalimbali za watu atakazotembelea. Kipindi hicho kitarushwa kupitia Clouds Tv na tayari actress huyo ameanza kushoot kipindi hicho kama anavyoonekana pichani hapo juu. Irene Uwoya ni muigizaji mwingine aliyeamua kugeukia vipindi vya Tv pia ukiachilia mbali kuigiza filamu wengine ni Rose Ndauka na Wema Sepetu ambaye show yake kuhusu maisha yake halisi pia kitarushwa Clouds Tv kuanzia mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka huu.

WEMA SEPETU AFUTURISHA NYUMBANI KWAKE

WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHINAWATRA AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini. Akisalimiana viongozi wa Tanzania.... Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  akikagua gwaride maalum la heshima lililoandaliwa kwaajili yake mara baada ya kuwasili nchini. PICHA zaidi bofa READ MORE

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP-GABERONE -BOTSWANA

PICHA ZIKIONYESHA MANDHARI MBALIMBALI YA MJI WA TANGA.WALE WA TANGA MPO?

Maeneo ya Chumbageni

Maeneo ya Chumbageni

Bandari ya Tanga inavyoonekana kwa mbali

AHUKUMIWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA NA KUMZALISHA MWANAYE

Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe akiwa kizimbani.
Yusufu akificha sura yake asipigwe picha baada ya hukumu ya miaka 30.Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakati wakitoka mahakamani. Kushoto ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa. MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa). Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.

AFRICAN PRINT ROCKS!

SURA MBALIMBALI ZA MFALME WA MUZIKI WA POP,MICHAEL JACKSON

1

2


3
Kwa sura zaidi bofya READ MORE

MARIO BALOTELLI-MCHEZAJI ASIYEISHIWA VITUKO.PICHA ZINAJIELEZA HAPA!

Mario Balotelli,mbali ya kuwa mwanasoka mzuri uwanjani,ni mchezaji anayeongoza kwa kuwa na vituko vingi. Je,unajua kuwa Mario ana mtoto?Fuatilia picha zake hapa kwani picha zenyewe zinaongea.


BILIONEA ALIYEMWAGIWA TINDIKALI DAR… HALI TETE

Na Mwandishi Wetu HALI ni tete kuhusiana na tukio la bilionea Said Mohamed Saad kumwagiwa tindikali, athari ni kubwa. Jinsi alivyoharibika inatia simanzi lakini kumpata mhusika wa unyama huo ni kitendawili kinacholitega Jeshi la Polisi Tanzania.
Rais Kikwete akimjulia hali mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Said Mohamed Saad. Said ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, yenye maduka mengi makubwa ya vitu vya nyumbani ndani ya Dar es Salaam na mikoa kadhaa ya Tanzania, anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini lakini mmoja wa watu waliomshuhudia, amefafanua jinsi hali ilivyo mbaya.