Thursday 11 July 2013

JB-SHIKAMOO MZEE MAJUTO

King MajutoWAKATI filamu yake mpya ya Zawadi Yangu ikiendelea kukimbiza sokoni kwa sasa, muigizaji nyota  wa filamu nchini, Jacob Stephen 'JB' yupo mbioni kuachia kazi nyingine iitwayo 'Shikamoo Mzee'.
JB anayefahamika pia kwa jina la 'Bonge la Bwana' alisema filamu hiyo mpya amewashikirikisha  wasanii wakongwe wa fani hiyo kama Chuma Suleiman 'Bi Hindu' na Amri Athuman 'King Majuto'.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mtunzi, mwandishi wa miswada, muongozaji na mtayarishaji filamu  alisema kuwa wasanii wengine walioshiriki filamu hiyo itakayoachiwa mwishoni mwa mwezi huu ni  Seleman Abdallah 'Barafu', Shamsa Ford na wakali wengine.
"Baada ya kuwapa mashabiki wangu 'Zawadi Yangu' safari hii wajiandae kupata burudani nyingine  kupitia 'Shikamoo Mzee' ambayo nimeigiza tena na King Majuto, Bi Hindu na wakali wengine,"  alisema.
JB alisema amejiwekea malengo kwamba kila mwaka afyatue filamu moja na mkongwe King  Majuto na kazi hiyo inakuja baada ya makamuzi makubwa waliyofanya kwenye 'Naenda kwa  Wanangu'.
"Kwa walioiona 'Naenda kwa Mwanangu' wanaweza kuelewa maana ya makamuzi, ila safari hii ni  funika bovu kwani mkongwe huyu akishirikiana na Bi Hindu wamefanya majambo yasiyo ya  kawaida wakisapotiwa na mimi mwenyewe JB, Shamsa Ford, Barafu na wengine," alisema JB.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...