Wednesday 17 July 2013

MATATANI KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO BILA KIBALI

Mlima Kilimanjaro
 Raia wawili kutoka nchi jirani ya Kenya, wamekamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa eneo la Mlima wa Kilimanjaro bila ya kuwa na kibali cha kupanda mlima huo.
Taarifa iliyotolewa na Tanapa kupitia idara yake ya uhusiano na kusainiwa na Meneja uhusiano wake, Paschal Shelutete imesema raia hao wa Kenya wanatoka eneo la Taveta na wanasadikiwa kuingia hifadhini kwa kupitia vichakani na walikamatwa kati ya eneo la Lango la Marangu na Kituo cha Mandara.

Shelutete alisema suala hilo la kukamatwa kwa watu hao, tayari limefikishwa katika Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha, katika hatua nyingine watu watatu wa familia moja wamekamatwa na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha wakishirikiana na polisi kwa tuhuma za kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni mifupa mitatu ya twiga yenye uzito wa kilo 10.4 na mfupa mmoja wa tembo wenye uzito wa kilo tano.
Watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Kisongo Lasite kutokana na taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watuhumiwa kumiliki nyara hizo.
Vilevile askari wa Hifadhi ya Taifa Arusha, wamemkamata mtu mmoja kwa kukutwa na silaha aina ya Shotgun namba C 139415 inayoaminika kutumika kwa ujangili.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...