Tuesday, 16 July 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA HUDUMA MPYA YA BENKI YA POSTA IITWAYO TPB POPOTE

Mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete akizindua huduma mpya ya Benki ya Posta iitwayo TPB
POPOTE mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
Rais Jakaya Kikwete akijaza fomu yake ya huduma hiyo mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Pichani kulia ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kushto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
 Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.
  Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa kadi yake mpya ya huduma mpya TPB POPOTE  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki  ya Posta Bw.Moshingi ,mara baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi mapema leo .




  Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya 
Picha pamoja.
Rais Jakaya Kikwete akiondoka mara baada ya kuzindua huduma mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.

CHANZO: Full shangwe

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...