Tuesday 23 July 2013

WATANZANIA WASUMBULIWA NA BALOZI ZA EU NCHINI!



-Ni juu ya upatikanaji wa VISA za safari

Imebainika kuwa balozi za  nchi za ulaya zilizopo hapa nchini, zikiwemo balozi za Ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi na nyinginezo,
zimekuwa zikiwasumbua sana raia wa Tanzania wanaohitaji Visa za kusafiria kwenda katika nchi za Ulaya.



Pamoja na kuwa Watanzania wanatimiza masharti yote yanayohitajika katika kuomba Visa lakini balozi hizo zimekuwa bado zikiwawekea vikwazo visivyo katika sheria za maombi ya Visa. Mfano Mtanzania anapo omba Visa ubalozini atapeleka barua ya mwaliko na bima, pamoja na Bank statment, barua ya kazini, Pay in sleep za mishaara.
Heti bado Ofisa Ubalozi anadai barua nyingine itoke kwa mwenyeji kuonyesha mlijuana vipi na mgeni Mtanzania!
Kwa kweli hakuna uhusiano mzuri katika ya raia na maofisa wa visa wa balozi za EU nchini Tanzania.
Serikali inaweza kuwa na uhusiano mzuri na balozi hizo lakini raia wa Tanzania hawathaminiwi kabisa na balozi za EU hapa Tanzania.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...