Wednesday 10 July 2013

ZIARA YA WAZIRI WA UJENZI DKT, JOHN MAGUFULI KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA JIJINI DAR

Muoenekano wa ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni katika awamu ya kwanza ambalo umekamilika kwa asilimia 47, katika mradi huo ujenzi huo utagharimu sh.Bilioni 214,kati ya fedha hizo asilimia 60 zimetolewa na Shirika la Hifadhi ya Mfuko wa Jamii (NSSF). Picha hii imepigwa jana wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli hayupo pichani wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Dar es Salaam ikiwemo ya ujenzi wa daraji hili.
Waziri wa Ujenzi Dkt, John Magufuli, (mwenye kofia ya pama) akiongea na Diwani wa kata ya Mwenge Dkt. Julian Bujugo(aliemshika begani) wakati ya ziara yake .
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi waliokuwa katika ziara yake.
Muonekano wa ujenzi unaoendelea wa ujenzi wa barabara ya Davis Corner- Vituka - Jet Corner.
Baadhi ya ujenzi wa vituo vya mradi wa Mabasi ya mwendo kasi (DART) barabara ya eneo la Ubungo,Mwembechai , Jangwani na Kivukoni vikiendelea.
Sehemu ya muonekano wa kituo cha mabasi ya mwendo kasi eneo la Kigamboni.
Ujenzi wa Daraja katika maeneo ya Tegeta wilaya ya Kinondoni ukiendelea. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...