Monday, 12 August 2013

KUMBUKUMBU YA MAMA YETU FATUMA NINDI LEO TAREHE 12 AUGUST

Siku kama ya leo  tarehe 12 augusti mwaka 2010 mama ulitutoka.Siku hii ilikuwa ngumu sana kwetu kwani si rahisi kuelezeka.
Mama kwetu ulikuwa si mama tu bali mshauri na rafiki yetu mkubwa.Huku mshauri na rafiki bora kwetu tu bali hata kwa marafiki na majirani zako ambao wote wanakukumbuka kila siku.
Kila nafsi itaonja mauti bali kwetu sisi wanao tunaona kama umetutoka mapema sana na katika muda ambao tulikuwa tunakuhitaji zaidi.
Mama tulikupenda sana ila Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi yetu na ndiyo maana akakutwaa.
Tutaendelea kutenda yale mema yote uliyotufundisha kubwa likiwa ni UPENDO.
Unakumbukwa na sisi wanao Anna,Patrick na James bila kusahau wajukuu zako  Browne Kelvin(Costa) na Evelyn.
MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI MAMA,AMEN.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...