Tuesday 20 August 2013

LIYUMBA AKWAA BALAA JIPYA

Hamida Hassan na Gladness Mallya
MNAMKUMBUKA aliyekuwa kigogo wa Benki Kuu ya Tanzania aliyefungwa jela miaka miwili kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa mali za umma, Amatus Joackim Liyumba? Basi amekwaa balaa jipya, Uwazi linajua kila kitu.
Amatus Joackim Liyumba.
Liyumba na mwanamke aliyedai ni mke wake, Aurelia Paulo Ngowi wamefikishana Mahakama ya Kinondoni, Dar kisa kikidaiwa ni mzee huyo kumtaka mwanamke huyo kuondoka haraka kwenye nyumba anayoishi na watoto wao wawili.


Nyumba hiyo ipo Mbezi ya Afrikana, jijini Dar. Mbali na kuwa makazi, lakini sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ni Hoteli Amjen yenye kupata wateja kila siku.
Jina la Amjen linadaiwa ni muuganiko wa majina ya Amatus na Jennifer ambaye ni mtoto mmoja kati ya hao wawili wa mzee huyo.
Aurelia ndiye aliyekimbilia mahakamani kuomba msaada ambapo shauri lake lilifunguliwa kwa namba 59, 2013 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Rugemalira.
Baada ya ombi hilo, mahakama ilimwamuru Liyumba kumwacha mkewe na watoto hao waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka shauri hilo litakapotatuliwa kisheria.
Haikujulikana mara moja kama Liyumba anataka mkewe na watoto waondoke kwenye nyumba hiyo na yeye kwa sasa anaishi wapi.
Jitihada za kumtafuta zilifanyika, simu yake ya mkononi haikuwa hewani huku ikidaiwa kwamba namba husika haitumii tena.
Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia Uwazi kwamba, kwa sasa Liyumba anaishi Kinondoni, Dar es Salaam lakini kupatikana kwenye simu ni ishu nyingine.
CHANZO: GPL

1 comment:

  1. huyu mama anakaa ubungo kwenye maflat na anajulikana huko..sasa huko mbezi amekaa lini! jamani hii story ni ya uongo! mchaga kazaa nae miaka 30 uliyopita na liyumba alioaga mke mmoja tu na alikuwa chotara wa kijerumani na ameshafariki. Naijua hii familia kwa ukaribu sana. huyu mama anataka tu attention. ashindwe ! eti na watotowke wawili wakati liumba ana watoto kama 10hivi! na mamazao tofauti kama watano.. alizaa nao lakini hakuwahi kuwaoa

    ReplyDelete

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...