Saturday, 10 August 2013

Oprah Winfrey abaguliwa nchini Uswis.

oprah
Oprah Winfrey

Mwanamke maarufu zaidi duniani Oprah Winfrey amekumbana ana kwa ana na kile anachokiita kitendo cha Ubaguzi wa rangi nchini Switzerland baada ya muuza duka mmoja kukataa kumuuzia mkoba wa kike wa mkononi na kumwambia kuwa hangeweza gharama yake.

Oprah ambaye ametajwa katika vitabu vya Forbes kama mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa duniani na mmoja wa watu tajiri zaidi amedai kuwa msichana aliyekuwa akiuza hapo dukani alimdharau kutokana na rangi yake.

Wiki iliyopita nchi hiyo ilitangaza sheria katika baadhi ya mabaraza yake ya miji kuwa wahamiaji wa nje hawataruhusiwa kutangamana na raia wenyeji hasa katika maeneo ya umma kama vile mabwawa ya kuogelea, uwanja wa michezo na hata kanisani.Uswis imejikuta katika kizungumkuti na wanaharakati wa haki za binadamu.

Sasa madai haya ya Oprah yanatoa taswira mbaya zaidi ya jinsi hali ilivyo nchini humo kuhusu ubaguzi wa rangi.
Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema kuwa hii ni ishara ya kuwa na ubaguzi ule uliowahi kutokea kwa muda mrefu huko Afrika Kusini.
Oprah amesema kuwa aliondoka dukani hapo taratibu bila kufanya vurugu lakini amesikitika kuona kuwa bado ubaguzi wa rangi unaendelea na kuenea.
Mwaka jana pekee Oprah alikuwa na fedha jumla ya dola za Kimarekani milioni sabini na saba na amesifiwa kuwa mfanyibiashara tajiri, ambaye pia anamiliki shirika lake binafsi la utangazaji na anafadhili miradi mingi ya misaada katika pembe mbali mbali za dunia.
Alipata umaarufu wake kutokana na kipindi chake cha Oprah Winfrey Show kilichooneshwa nchi nyingi.
Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Zurich anasema kuwa kipindi hicho hakijawahi kupeperushwa katika runinga za Switzerland na huenda sio wengi wanaofahamu Oprah ni nani huko.
Oprah alikwenda Uswis kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Tina Turner.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...