Sunday, 13 October 2013

HABARI YA KUSIKITISHA: HAWAKUOMBA KUJA DUNIANI KUTESEKA

Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha 
Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Agustino Steven (8) akipika mchicha
Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula 
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe
Unga pamoja na maharaja
Hili ndilo sanduku lao
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi matano bila huduma za msingi.

Watoto hao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine.

Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.

Aidha watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500 ambazo huzitumia kununua mahitaji ya nyumbani pamoja na kujipikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Amesema majirani pia waendelee kuwa karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao watakapopatikana kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida.



Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo pia alitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao  wa mbeyayetu.blogspot.com umebaini kuwa Wazazi hao wanatabia kama hiyo kutokana na kuwahi kumtelekeza binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Salome Steven ambaye hakuwahi kupelekwa shule hivyo kuachiwa jukumu la kuwalea wadogo zake.

Kutokana na ugumu wa maisha binti huyo katika harakati za kutafuta chochote kwa ajili ya wadogo zake ameishia kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake na yeye kukimbilia kwa rafiki yake.

Pia Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia limeamua kulifuatilia suala hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti ).
CHANZO: Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...