Tuesday 29 October 2013

MWILI WA BABA YAKE WEMA SEPETU, MAREHEMU BALOZI ISAAC SEPETU KUAGWA KESHO JUMANNE NA MAZIKO NI JUMATANO OKTOBA 30, 2013


Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu  enzi za uhai wake.

Mwili wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu utafikishwa nyumbani kwake eneo la Sinza Mori lililoko jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne October 29, 2013 kuanzia saa sita za mchana na mwili huo utaanza kuagwa kwenye mida ya saa nane za mchana na baada ya kuagwa mwili huo utafanyiwa maandalizi ya kusafirishwa kwenda Zanzibar siku ya Jumatano asubuhi tarehe 30, October 2013 na mwili wa marehemu ukifika Zanzibar, Unguja utapelekwa  kanisani kwa ajili ya maombi pia utapumzishwa kwenye makazi yake ya daima eneo la Mbozini, Unguja siku ya Jumatano October  30, 2013
Balozi David Kapya akisaini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Balozi  Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake eneo la Sinza Mori jijini Dar es salaam leo Jumatatu October 28, 2013
Mtoto wa maheremu na pia msemaji wa familia Aman Isaac Sepetu akizungumza na vyombo vya habari leo nyumbani kwa marehemu






















Balozi David Kapya akibadilishana mawazo na ndugu, jamaa na marafiki kwenye msiba wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake maeneo ya Sinza Mori


Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba


HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ISAAC
ABRAHAMU SEPETU
Balozi Isaac Abraham Sepetu alizaliwa October 15, 1943, ni mzaliwa wa Tabora ila alikulia Zanzibar na alikuwa ni mkaazi wa Zanzibar mpaka mauti yanamfika.
 
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alipata elimu yake ya msingi na sekondari  katika shule ya St.joseph’s  kwa sasa inaitwa Tumekuja huko Zanzibar mnamo mwaka 1952 hadi 1963, vilevile aliweza kujiunga na chuo kikuu huko Berlin nchini Ujerumani mwaka 1964 hadi 1970 alisomea Shahada ya Uchumi, Marehemu alikuwa anauwezo wa kuongea lugha tatu (3) kwa ufasaha ambazo ni ;- kiswahili, kingereza  na kijerumani.

KAZI
Alianza kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1971 hadi 1972 kama Mkuu wa Bizanje Msaidizi na pia alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ikulu. Baada ya hapo mwaka 1972 hadi 1977 alikuwa Naibu Waziri Mambo ya Nje  katika serikali ya Muungano Zanzibar, mnamo mwaka 1977 hadi 1979 Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu  alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji, Ilipofika mwaka 1979 hadi 1982 alikuwa Waziri wa Utalii na Maliasili.
Marehemu Balozi  Sepetu mwaka 1982 hadi 1989 alipewa nafasi ya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Moscow na mwaka 1989 hadi 1990 alikuwa Balozi wa nchi ya Zaire, Kinshasa

Katika Serikali ya Mapinduzi Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Waziri wa Nchi, Mipango pia alikuwa Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na pia alikuwa Katibu , Kamati ya Pamoja(IPC) CCM/CUF, Zanzibar Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa mbunge wa bunge la Afrika ya Mashariki
Uzoefu wa Kisiasa Mwaka 1977 hadi 2005 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi.
CHANZO: KAJUNA BLOG

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...