Tuesday 19 November 2013

AJALI ILIYOUA WATU SABA NA KUJERUHI WATANO MKOANI MORO LEO ASUBUHI

Toyota Noah yenye namba za usajili T502 AUP iliyokuwa ikitoka wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini baada ya kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB.
...Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.
...Muonekano wa Toyota  Noah kwa nyuma baada ya ajali.
...Ndani ya Toyota Noah baada ya ajali.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora baada ya kugongana uso kwa uso na Toyota Noah  yenye namba za usajili T502 AUP.
Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB baada ya ajali.

WATU saba wamekufa papo hapo kwenye ajali mbaya iliyotoka leo alfajiri katika kijiji cha Dakawa - Sokoine Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyohusisha gari ya abiria aina ya Noah yenye namba za usajili T 502 AUP iliyokuwa ikitoka Wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129 AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora.

Watu saba wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni mbaya. "Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa uso" Alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
                                              (HABARI NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...