Tuesday 19 November 2013

AY ASEMA HATOCHANGISHA MICHANGO KWENYE ARUSI YAKE

Ambwene Yesaya aka AY amesema hatochangisha michango kwenye harusi yake siku za usoni.
IMG_7501
AY akiwa na mchumba wake, kwenye red carpet ya show yake ya
Road to CHOAMVA 2013, Club Bilicanas Jumapili iliyopita


AY ambaye yupo Nairobi, Kenya alikoenda kufanya video ya ‘Jipe Shavu’ aliyofanya na Fid Q, alikuwa akiongea na Mzazi William Tuva katika kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya nchini Kenya leo.

“Nadhani huu ni wakati wangu pia wa kutimiza zile hatua za maisha. Inafika time inabidi uwe na mtu ambaye anaweza akakushauri katika vitu,. Unajua unapozidi kukua na mambo mengi yanakuwa yanafanyika, let’s say una plans kibao, una vitu ambavyo unataka kuvifanya mbele. So lazima uwe na mtu ambaye ni mkono wako wa kushoto ambaye anaweza akakushauri.

So yupo, nilijaribu kufanya research kidogo, nikapata mchanganyiko wa Sheli Sheli na Myemen,” alisema AY.

Hata hivyo AY amesema hatochangisha michango kwenye harusi yake.
Msikilize hapa.
 CHANZO: Bongo5

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...