Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kiongozi mwandamizi wa chama cha NCCR Mageuzi, marehemu Dr. Sengondo Mvungi huko Mbezi Kibamba jijini Dar es Salaam leo mchana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya Marehemu Dkt.Sengondo Mpicha na Freddy Maro.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na
Rais Jakaya Kikwete (wapili kulia) wakiwa msibani leo nyumbani kwa
marehemu Kibamba Msakuzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Wengine
pichani kutoka kulia ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia (MB),
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph sinde Warioba,
jaji Mkuu Mstaafu, Augustino ramadhani, Waziri wa Katiba na Sheria,
Mathias Chikawe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Meck Sadik
Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Dkt. Sengondo Mvungi kuwasili Ijumaa, Novemba 15, 2013
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za
kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki
nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili
nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.
Aidha,
siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa
4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya
Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16,
2013.
Aidha,
Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba
17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa
ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18,
2013.
Dkt.
Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya
Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili
ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili
(MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Wakati huohuo,
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake
Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13, 2013) wameungana na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi eneo la Kibamba jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa
marehemu Dkt. Mvungi.
CHANZO: Pamoja pure
CHANZO: Pamoja pure
No comments:
Post a Comment