Wednesday 13 November 2013

MENO YA TEMBO YAKAMATWA KWENYE KONTENA LA FUTI 40 ZANZIBAR LEO


Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyoleo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Askari wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za Tembo katika makunia wakati wa zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Magunia haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya Zanzibar leo asubuhi. 
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo 


Baadhi ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na uzito kwa ujumla.
Operesheni ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata thamani yake halisi.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.
PICHA KWA HISANI YA ISSA MICHUZI
ANGALIZO: Kwa spidi hii sijui kama kuna tembo atabakia.Inasikitisha sana.Tuacheni kununua vitu vinavyotengenezwa na meno ya tembo kuwanusuru tembo wetu!INAWEZEKANA,CHUKUA HATUA SASA!

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...